Category talk:Petition Translations

From L'avenir de l'humanité

YALIYOMO

  • 1 Taarifa ya Usuli
  • 2 Viwango vinavyohitajika kote Ulimwenguni

o 2.1 Umri wa kadiri wa kuoa o 2.2 Umri wa kadiri wa kupata watoto o 2.3 Vigezo vya kuzaa o 2.4 Idadi ya mwisho ya watoto katika familia o 2.5 Muda wa kuzuia uzazi o 2.6 Muda wa sheria hii itakapotumika o 2.7 Adhabu kwa wanaokiuka o 2.8 Kikatili, kinyama na isiyo na huruma

  • 3 Chati ya kukua kwa watu Ulimwenguni
  • 4 Chanzo/Asili
  • 5 Masomo ya ziada
  • 6 Kutia sahihi ombi

TAARIFA YA USULI

KWA : Watu wa Ulimwenguni, Ulimwengu na viumbe vilivyomo ndani yake wamekuwa wakitaaabika kutokana na maovu yanayotekelezwa na mwanadamu yeye binafsi. Maovu haya yaliyopo kwa hivi sasa yataendelea kuongezeka hadi pale kila kitu kitakapoharibika.

Idadi ya watu waliopo ulimwenguni wameathirika na baa la njaa, ukosefu wa nguvu za kawi, majanga, uchafuzi wa mazingira , upotovu na ukosefu wa maadili, ugaidi, udikteta, kutokuwepo kwa serikali huru, utumwa, ongeeko la vifaa vya uchafuzi, ubaguzi wa rangi, uhaba wa chakula, uharibifu wa misitu, uchafuzi wa maziwa, mito, chemchemi na hata bahari, chuki dhidi ya watu wanaotafuta hifadhi, kutoka kwa mnunurisho wa nuklidi za redio(radioactive emissions), uchafuzi wa maji, hewa, mimea, chakula, binadamu na hata wanyama kwa njia ya kemikali . Uhalifu, mauaji, mauaji ya halaiki, mauaji bila ya kukusudia, unywaji wa pombe, chuki dhidi ya wageni,ukandamizaji, chuki dhidi ya binadamu mwengine, kuwepo kwa wafuasi wa siasa kali, ufuasi wa madhehebu au kikundi Fulani, matumizi ya madawa ya kulevya , kuwepo kwa idadi kubwa ya watu kupita kiasi, vita, ghasia, mateso, adhabu ya kifo usimamizi mbaya, machafuzi ya maji, kuondolewa kwa aina fulani ya mimea, chuki, wivu, ukosefu wa mapenzi, ubinadamu bandia, ukosefu wa makao, ongezeko la magari, uharibifu wa ardhi, ukosefu wa ajira, kufifia kwa vituo vya afya, kukosekana kwa vituo vya uangalizi kwa watu wazima, uharibifu wa mazingira, kufifia kwa vituo vya kusafisha maji taka na ukosefu wa sehemu za kuishi miongoni mwa matatizo mengine. Na licha ya juhudi nyingi zinazofanywa, matatizo ya binadamu hayapungui badala yake yanaendelea kuongezeka kadiri idadi ya watu inavyoongezeka kote ulimwenguni.

Maovu ya binadamu yaliyopo na yale yataendelea kufanyika yanatokana na ongezeko la binadamu ulimwenguni ambao wanaongezeka kiholela. Hali hii inatoa maongozo ya jinsi ya kukabiliana na maovu na kutafuta suluhu yake kwa njia ya kutafuta asili na usuli wake pamoja na kuliangamiza kabisa chimbuko la maovu hayo. Ongezeko kuu la watu ulimwenguni ni sharti lipunguzwe. Na kufanikisha lengo hili kwa njia za kibinadamu ni kuweka misimamo mikali inayofaa kutiiwa na kufuatwa ya upangaji wa uzazi ambao utaruhusu tu wanandoa wa umri fulani, kuwa na idadi maalum ya watoto kwa mujibu wa mapendekezo yaliyowekwa.

Utaratibu huu ni sharti utekelezwe na pasiwepo sababu au hoja ya kuipinga aidha kwa njia ya hofu au kwa kutoa madai yasiyokuwa na msingi wowote hususan kutoka kwa watu wapumbavu wanaodai kuwa kwa ajili ya kuwa na jeshi, au kwa misingi ya kidini, kijamii au hata kwa misingi bandia ya kutetea haki za kibinadamu ni sharti kuwepo kwa idadi kubwa ya watu ulimwenguni sawaia na kusema kuwa upangaji uzazi kunaenda kinyume na maadili ya kidini na kutaja tendo hilo kama unyama na udhalimu kwa binadamu miongoni mwa sababu nyengine zisizokuwa na msingi. Madai haya ya kipuuzi hutolewa na watu wenye ubinafsi au dhehebu lenye mawazo finyu ambao ni miongoni mwa watu wasiofaa kuishi kwa sababu ni watu wasiokuwa na miongozo ya hulka za kimaisha na ukweli kuhusu busara za kuishi.

Huku kukiwa na idadi ya makisio ya watu billioni 6.5 ulimwenguni katika kipindi cha mwaka wa (1998), takwimu huu inaonyesha kuwa ulimwengu hauwezi kuhimili idadi hii kubwa ya watu sawia na kutoa lishe kwao kwa kufuata taratibu za mazao asilia na kufuata vigezo vya afya bora.

Kwa msingi huu, kuna haja ya kuwepo ulimwengu usiokuwa na uharibifu wa rasilimali zake ili kuwezesha uzalishaji wa chakula zaidi, na ulimwengu ambao viumbe wanaoishi ndani yake hawatakufa kwa njaa. Ukweli ni kwamba dunia ni sayari ya maajabu sana , lakini ina uwezo wa kuwakimu na kuwalisha kwa wingi viumbe 529 millioni waliomo ndani yake. Walimwengu nao kwa upande wao wamechangia kuwepo kwa idadi kubwa ya watu na kulazimika kushambulia mazao yote ya matunda na mboga, na ili kufidia upungufu huu mazao hulazimika kunyunyuziwa kemikali ili kutoa vyakula vya mvyauso(hybrid) Na kama hili halitoshi uharibifu wa dunia umekuwa unaongezeka kila uchao,ikiwemo ongezeko la uhitaji wa mali ghafi na mambo mengineyo yanayochangia kuwepo kwa ongezeko la watu zaidi. Hakuna anayezungumzia uharibifu wa ardhi inayolimika kutokana na umaluuni wa kuwepo kwa watu kupita kiasi, na wala hakuna anayezungumzia matumizi ya kemikali zenye sumu, upanuzi wa majumba na mambo mengineyo yenye athari zaidi. Vyakula vinavyotumika vimerashiwa kemikali na vingi vinayotumika wakati huu huwa ni vile vinavyozalishwa kwa njia ya kemikali , swala ambalo halijadiliwi kamwe.

Ongezeko la watu kupita kiasi pia huchangia matatizo ya kikabila, na zaidi ni kwamba ongezeko hili ndilo linalochochea kuwepo kwa hali hii. Miongoni mwa mambo yanayochochewa na ongezeko la watu ni pamoja na watu kuhama kutoka eneo moja hadi jengine, vita , umwagikaji wa damu na mauaji. Na kutokana na ongezeko la watu ulimwenguni watu hulazimika kujifinyilia mahala pamoja na kupigania nafasi chache yenye uhaba inayozozaniwa na watu wengi zaidi. Kwa sababu hii hali kadhaa za kutanisha haziwezi kuepukika ambapo watu wa mataifa tofauti, makabila, dini, ushawishi, maoni na falsafa mbalimbali hujumuika pamoja na kuanza mvutano wa kung’ang’ania nafasi chache iliyopo na kwenye hali hii ya maingiliano ya karibu hudhihirika jambo linalopelekea migongano na kutoelewana.

Kwa mantiki hii,vita, umwagikaji wa damu, mauaji na hata kuhama kutoka eneo moja hadi jengine hutokea. Swala la kuhama kutoka eneo moja peke yake huchangia kuwepo kwa matatizo zaidi kote ulimwenguni. Kwa mfano, wakimbizi hawaachi makaazi yao waliyoyazoea na kutafuta makazi mapya kwenye sehemu nyengine katika taifa lao. Badala yake wengi wao hutorokea kwenye mataifa ya kigeni au hata kwenye mataifa yaliyo imara kiuchumi na yenye maendeleo ikilinganishwa na mataifa wanayotoka. Hii ina maana kwamba maelfu, makumi ya maelfu, na hata malaki au hata mamilllioni ya wakimbizi hutoroka ghafla kutoka kwenye makao yao na kufurika kwenye mataifa ya kigeni yaliyo na ustawai zaidi. Na pahala pake, mataifa haya hufurika na wakimbizi ambao huchangia matatizo yasiyokadirika. Na mataifa yanayowapokea wakimbizi hawa hulazimika kutumia mabilioni ya dola za Marekani ambazo hutolewa na mataifa fadhili kuwakimu wakimbizi hawa, na fedha hizi hulazimika kutoka kwa wananchi wanaotozwa ushuru.

Matatizo ya viumbe waliopo ulimwenguni kwa hivi sasa yanaweza kutatuliwa kupitia njia ya kuzuia uzazi kwa malengo maalum, na kuweka idadi ya binadamu katika kiwango kinachohitajika na ulimwengu kwa ujumla.

Je, kudhibiti uzazi kwa njia ya mpango wa uzazi ni njia ya kinyama na ya kikatili isiyokubaliana na maadili? La! Kimsingi ni kuwa mtu atakapoanza kuzipima hoja hizi iwapo hajafanya hivyo basi ukweli utambainikia kwamba uhalisia umo katika hoja tuliyoijadili hapo awali kwamba, upangaji wa uzazi ndio njia ya sawa.

Ni kwa watu pekee wasiokuwa na maadili ambao hushitadi kwenye uwongo na kuupinga ukweli. Watu wa aina hii huongozwa na madhehebu ya uwongo na kuwanyima upeo wa fikra za kiafya, zenye uwezo wa kutoa maamuzi ya busara na fikra za dhati na vitendo vya kweli. Watu wa aina hii hutawaliwa masikitiko na kujihurumia , na huwa na wingi wa akili dhaifu, badala ya kuwa na uwezo wa kuhisi maono ya mtu mwengine na maisha kwa ujumla. Nidhamu ya kweli kuhusu maisha hupotea kwa watu wenye mawazo finyu ambao hueneza kasumba za uwongo na kuenea kwa kasi kubwa mno.

Je ni ukatili na unyama iwapo sheria na maongozo ya ulimwengu yatakapofuatwa? Jawabu ni La. Hata hivyo ni kinyama na kinyume cha maadili pale binadamu anapochangia kwenye kuongezeka kwa idadi kubwa ya watu na kuhamasisha kuwepo kwa ongezeko hilo bila ya kujali athari za kuzaliwa kwa mamillioni na mamillioni ya watoto wapya watakaozaliwa. Na kwa kushindwa kuweka njia muafaka za kudhibiti uzazi kwa mpango kutokana na mawazo finyu na akili punguani mwanadamu yeye mwenyewe huchangia kwenye matatizo mengi zaidi ambayo huwa makubwa zaidi na mwishowe huwa vigumu kuyatatua. ZINGATIA : Hii ni sehemu tu kati ya sehemu kamilifu ambayo unashauriwa kuisoma ili upate ufahamu kamilifu.

VIWANGO VYA KIMATAIFA VINAVYOHITAJIKA

Hii ni mojawapo ya uwezekano miongoni mwa mifano mingi! Viwango na mbinu hizi zinaweza kutumika kwa kila mtu aliyepo ulimwenguni isipokuwa kwa makabila madogo ya kiasili ambayo yamekuwa yakidumisha mbinu zao za kiasili za kuzuia uzazi tangu jadi. Umri wa kadiri kwa ndoa

  • Mke: Miaka 25
  • Mume: Miaka 30

Umri wa kadiri wa kupata watoto

  • Mke : Miaka 28
  • Mume: Miaka 32

Vigezo vya kupata watoto

  • Kuwepo kwa ndoa katika kipindi cha miaka 3
  • Thibitisho la ndoa yenye masikilizano na utangamano
  • Thibitisho la nidhamu ya hali ya juu kati ya wanandoa
  • Thibitisho la kuweza kuwalea watoto
  • Thibitisho la afya njema na pasiwepo maradhi ya maambukizi na

yale ya kiukoo, pasiwepo matumizi sugu ya madawa ya kulevya pamoja na historia ya kushiriki ulevi n.k

  • Kusiwepo maingiliano na ushirikiano na makundi haramu.

Idadi ya watoto kwa wana ndoa

  • Watoto 3 kwa kila ndoa

Muda wa kuzuia uzazi Miaka 7 marufuku ya kuzaa kote ulimwenguni Mwaka 1 makubaliano ya kuzaa (kwa idhini) Miaka 7 kote ulimwenguni, marufuku kamili ya kutozaa Mwaka 1 idhini ya kuzaa (kwa kupata kibali ) kutekelezwa kwa mpango huu hadi pale idadi ya watu ulimwenguni imetimu kiwango cha wastani kinachokubalika cha watu 529,000,000 kote ulimwenguni Matokeo yake: Viwango kuhusu idhini ya kuoa na kuzaa viendelee kutekelezwa , lakini kipindi cha miaka 7 cha kuangalia kima cha uzazi kuondolewa.

Sheria hii kutumika

  • Watoto 3 kwa kila ndoa (au watoto 3 wa kupanga)

Adhabu kwa wanaokiuka 1. Faini ya kiasi sawa na mishahara ya miaka 10 kwa wote waliokiuka. 2. Kuhasiwa kwa wakosaji wote wawili 3. Kuhasiwa kwa wahalifu wa ubakaji n.k Na wahalifu hawa kutengwa kutoka katika jamii pamoja na jinsia katika kipindi kilichosalia cha maisha yao. 4. Watoto wa wahalifu hao kuchukuliwa kutoka kwa wazazi wao na badala yake watoto hao kulelewa na wazazi wa kupanga au serikali. ZINGATIA! Tafadhali soma maelezo yenye ufafanuzi kuhusu mpango wa uzazi katika kipindi cha miaka saba ambayo hutolewa kwenye kijitabu chenye maelezo kuhusu ongezeko la watu- kijitabu hiki ni #3! KIKATILI NA ISIYO NA HURUMA Ni kitu gani ambacho ni cha kikatili, kinyama na kisichokuwa na huruma kwa binadamu mwenzako na maisha kwa ujumla? 1. Ulimwengu unashamiri na ongezeko la watu, ambako njaa na majanga na vifo vya kikatili vimetawala, ulimwengu huu pia ni mahala ambako vita, mauaji, umwagikaji wa damu, mateso na hata adhabu ya kifo inatekelezwa kila siku sawia na visa vya ubakaji, uhalifu, chuki, maradhi,uharibifu na ulanguzi wa madawa; chuki zimeenea dhidi ya viumbe, siasa kali,uwongo na hadaa unadhihirika; pia ni mahala ambako mamilioni ya watu hufariki kila siku,na wengine kutaabika na hata kufariki mikononi mwa wale wanaowatesa na kuwaua, na wengine kutaabika kutokana na baa la njaa miongoni mwa matatizo mengine. AU 2. Ulimwengu wenye idadi ya wastani ya watu, huwa na maovu machache na matatizo pia hupungua. Ulimwengu wa aina hii huwa hautawaliwi na hofu ya vita na majanga na badala yake mahala pake kuchukuliwa na kiunganishi cha amani kote ulimwenguni. Hali hii husitisha kuishi kwa hofu na kutoa nafsi ya maisha ya mapenzi, yenye uelewano miongoni mwa mengi. Kwanini basi hutafakari aina ya ulimwengu ungelipenda kuishi ndani yake? Na jee ubinadamu wa dhati na wenye mapenzi hupiku kila aina ya uwongo?Na juu ya yote hayo jiulize: "Ni ulimwengu wa aina gani ninaotaka watoto wangu na watoto wa watoto wangu kuishi?" Billy CHATI YA KUKUA KWA IDADI YA WATU DUNIANI Kulingana na uchunguzi uliofanywa na shirika la FIGU, kumekuwa na ongezeko la idadi ya watu kote ulimwenguni na idadi hii imekuwa ikikua na kuongezeka kila siku kama ifuatavyo; Ustawi wa kukua kwa idadi ya watu duniani (kati ya kipindi cha miaka 2004 iliyopita ) Kipindi Mwaka wa kwanza Mwaka jana Kukua/Idadi Kamili

1-500 102,465,703 198,847,080 96,381,377 501-1000 198,847,080 293,408,074 94,560,994 1001-1300 293,408,074 374,079,611 80,671,537 1301-1500 374,079,611 406,100,043 32,020,432 1501-1600 406,100,043 463,618,432 57,518,389 1601-1700 463,618,432 536,718,004 73,099,572 1701-1800 536,718,004 892,333,410 355,615,406 1801-1900 892,333,410 1,660,990,034 768,656,624 1901-1905 1,660,990,034 1,689,987,973 28,997,939 1906-1910 1,689,987,973 1,810,900,001 120,912,028 1911-1915 1,810,900,001 1,844,760,039 33,860,038 1916-1920 1,844,760,039 1,912,000,432 67,240,393 1921-1925 1,912,000,432 2,008,401,932 96,401,500 1926-1930 2,008,401,932 2,207,034,890 198,632,958 1931-1935 2,207,034,890 2,350,481,002 143,446,112 1936-1940 2,350,481,002 2,400,389,101 49,908,099 1941-1945 2,400,389,101 2,550,108,498 149,719,397 1946-1950 2,550,108,498 2,600,047,000 49,938,502 1951-1955 2,600,047,000 2,784,382,444 184,335,444 1956-1960 2,784,382,444 3,050,382,081 265,999,637 1961-1963 3,050,382,081 3,250,798,000 200,415,919 1964-1966 3,250,798,000 3,500,100,000 249,302,000 1967-1969 3,500,100,000 3,700,641,801 200,541,801 1970-1972 3,700,641,801 3,783,847,320 83,205,519 1973-1975 3,783,847,320 3,889,992,910 106,145,590 1976-1978 3,889,992,910 4,090,799,983 200,807,073 1979-1981 4,090,799,983 4,604,031,892 513,231,909 1982-1984 4,604,031,892 4,800,411,000 196,379,108 1985-1987 4,800,411,000 5,149,979,380 349,568,380 1988-1990 5,149,979,380 5,367,887,093 217,907,713 1991-1993 5,367,887,093 5,876,884,097 508,997,004 1994-1996 5,876,884,097 6,204,008,014 327,123,917 1997-1999 6,204,008,014 6,634,101,302 430,093,288 2000-2002 6,634,101,302 6,905,000,109 270,898,807 2003-2005 6,905,000,109 7,503,846,002 598,845,893 Kukua kwa idadi ya watu duniani(kila mwaka,siku, saa na sekunde) Kipindi Muda( Miaka) Kukua/Idadi Kamili Kwa Mwaka Kwa siku Kwa saa Kwa sekunde 1-500 500 96,381,377 192,763 528 22 0.01 501-1000 500 94,560,994 189,122 518 22 0.01 1001-1300 300 80,671,537 268,905 737 31 0.01 1301-1500 200 32,020,432 160,102 439 18 0.01 1501-1600 100 57,518,389 575,184 1,576 66 0.02 1601-1700 100 73,099,572 730,996 2,003 83 0.02 1701-1800 100 355,615,406 3,556,154 9,743 406 0.11 1801-1900 100 768,656,624 7,686,566 21,059 877 0.24 1901-1905 5 28,997,939 5,799,588 15,889 662 0.18 1906-1910 5 120,912,028 24,182,406 66,253 2,761 0.77 1911-1915 5 33,860,038 6,772,008 18,553 773 0.21 1916-1920 5 67,240,393 13,448,079 36,844 1,535 0.43 1921-1925 5 96,401,500 19,280,300 52,823 2,201 0.61 1926-1930 5 198,632,958 39,726,592 108,840 4,535 1.26 1931-1935 5 143,446,112 28,689,222 78,601 3,275 0.91 1936-1940 5 49,908,099 9,981,620 27,347 1,139 0.32 1941-1945 5 149,719,397 29,943,879 82,038 3,418 0.95 1946-1950 5 49,938,502 9,987,700 27,364 1,140 0.32 1951-1955 5 184,335,444 36,867,089 101,006 4,209 1.17 1956-1960 5 265,999,637 53,199,927 145,753 6,073 1.69 1961-1963 3 200,415,919 66,805,306 183,028 7,626 2.12 1964-1966 3 249,302,000 83,100,667 227,673 9,486 2.64 1967-1969 3 200,541,801 66,847,267 183,143 7,631 2.12 1970-1972 3 83,205,519 27,735,173 75,987 3,166 0.88 1973-1975 3 106,145,590 35,381,863 96,937 4,039 1.12 1976-1978 3 200,807,073 66,935,691 183,385 7,641 2.12 1979-1981 3 513,231,909 171,077,303 468,705 19,529 5.42 1982-1984 3 196,379,108 65,459,703 179,342 7,473 2.08 1985-1987 3 349,568,380 116,522,793 319,241 13,302 3.69 1988-1990 3 217,907,713 72,635,904 199,002 8,292 2.3 1991-1993 3 508,997,004 169,665,668 464,837 19,368 5.38 1994-1996 3 327,123,917 109,041,306 298,743 12,448 3.46 1997-1999 3 430,093,288 143,364,429 392,779 16,366 4.55 2000-2002 3 270,898,807 90,299,602 247,396 10,308 2.86 2003-2005 3 598,845,893 199,615,298 546,891 22,787 6.33

CHANZO:

tabid/102/Default.aspx

ault.aspx MASOMO YA ZIADA

  • Kampeini dhidi ya ongezeko la watu
  • Tafsiri ya kipindi cha miaka 7-Year Cycle of Birth Rate Check
  • Bomu la ongezeko la watu

KUTIA SAHIHI OMBI HILI

Kwa kutia sahihi ombi hili unathibitisha kuwa utaunga mkono uzazi wa mpango hadi pale jumla ya idadi ya watu waliopo kote ulimwenguni itakapotimia 529,000,000.